Magoli mawili ya mshambuliaji Mbwana Samatta yameipeleka TP Mazembe fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika baada miamba hiyo ya Lubumbashi kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa pili wa nusu fainali uliopigwa jana jumapili huko Lubumbashi,Congo katika dimba la Stade du TP Mazembe.
Samatta alifunga magoli hayo dakika za 53 na 69 huku lile la tatu likifungwa na Muivory Coast Roger Assale dakika ya 71 na kuifanya TP Mazembe kuibuka na ushindi wa jumla wa magoli 4-2 baada ya kufungwa magoli 2-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliopigwa huko Sudan wiki mbili zilizopita.
Kufuatia ushindi huo TP Mazembe itavaana na USM Alger ya Algeria katika michezo miwili ya fainali inayotarajiwa kuchezwa kati ya Octoba 30 na Novemba 8 huku mshindi akitarajiwa kuvuna kitita cha $1.5m kama zawadi na nafasi ya kucheza michuano ya vilabu bingwa duniani mwezi disemba huko Japan.
0 comments:
Post a Comment