Timu za taifa za Hispania na Uswisi zimeungana na England kufuzu katika michuano ijayo ya Ulaya (Euro 2016) baada ya ijumaa usiku kuibuka na ushindi wa haja.
England ambayo ilikuwa imeshafuzu mapema kundi E iliitandika Estonia kwa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa Wembley mbele ya mashabiki 72,827.
Magoli ya England yamefungwa na Theo Walcott na Raheem Sterling na kuifanya England kuwa imeshinda michezo tisa kati ya tisa iliyocheza huku mchezo wake wa mwisho ikiwa ni dhidi ya Lithuania siku ya jumatatu.
Katika mchezo mwingine wa kundi E,Uswisi nayo imefuzu baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 7-0 dhidi ya San Marino kwa magoli ya Michael Lang, Gokhan Inler,
Admir Mehmedi, Johan Djourou, Pajtim
Kasami, Breel Embolo na Eren Derdiyok.
Kutoka Estadio Las Gaunas,Hispania imefuzu baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Luxembourg.Magoli ya Hispania yamefungwa na Santi Cazorla (2) na Paco Alcacer (2).
0 comments:
Post a Comment