Hakuna ugonjwa mbaya kama kukaa benchi,tena ukiwa mzima wa afya.Huna jeraha wala tatizo lolote.Uko benchi kwasababu umeshindwa kumridhisha kocha.Inauma sana.
Sikia Hii.Mlinzi wa kulia wa Arsenal,Mfaransa Mathieu Debuchy ameripotiwa kutaka kutimka klabuni hapo mwezi januari ikiwa ataendelea kukaa benchi.
Debuchy,30 ameongeza shauku ya kufanya uamuzi huo baada ya kutemwa katika kikosi cha Ufaransa kinachojindaa kucheza michezo miwili ya kujipima nguvu dhidi ya Armenia na Denmark wiki ijayo.
Kutoka Daily Mail habari zinasema Debuchy ambaye amepokonywa namba katika kikosi cha kwanza cha Arsenal na kinda Hector Bellerin,anahofia kuendelea kukaa benchi kutamnyima nafasi ya kuwemo katika kikosi cha Ufaransa kitakochokuwa mwenyeji wa michuano ya Euro 2016.Hivyo suluhu ni kuhamia katika klabu nyingine.
Debuchy alijiunga na Arsenal msimu uliopita lakini kutokana na majeraha ya mara kwa mara aliishia kucheza michezo kumi tu na msimu huu akifanikiwa kucheza kwa dakika 66 katika mchezo ambao Arsenal ilifungwa na West Ham.
0 comments:
Post a Comment