SIYO SIRI TENA.Taarifa za ndani toka klabu ya Chelsea zinadai kuwa kocha mkuu wa miamba hiyo ya ligi kuu ya England,Mreno Jose Mourinho anajiandaa kukipa makali zaidi kikosi chake ifikapo mwezi januari kwa kumsajili kiungo mahiri wa FC Porto Ruben Neves.
Taarifa zaidi zinadai tayari Chelsea imeshaandaa kitita cha nguvu cha £29m ili kuhakikisha inamnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka18 ambaye pia anawindwa kwa karibu na miamba ya Hispania na Ulaya FC Barcelona.
Chelsea imeongeza kasi katika mbio za kumnasa Neves baada ya kinda huyo kuonyesha kiwango kizuri na kuisaidia FC Porto kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi yao katika mchezo wa ligi ya mabingwa jumanne wa ligi ya mabingwa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment