Sergio Aguero ameiongoza klabu yake ya Manchester City kuifanyia mauaji makubwa klabu ya Newcastle United baada ya kuifungia magoli matano katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa katika dimba la Etihad,jijini Manchester jioni ya leo.
Newcastle United ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli dakika ya 18 kupitia kwa Alexander Mitrovic aliyefungwa kwa kichwa akiunganisha pasi safi ya Giorgio Wijnaldum.Baada ya kuingia kwa goli Manchester City iliamka na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 42 kupitia kwa Sergio Aguero ambaye aliongeza mengine dakika za 46,49,50,60 na 62 huku Kevin De Bruyne akifunga dakika ya 54.
Kufuatia ushindi wa leo Manchester City imerejea kileleni mwa ligi na kuishusha Manchester United ambayo itacheza kesho jumapili dhidi ya Arsenal katika dimba la Emirates.
Matokeo mengine ya michezo ya leo jumamosi
Aston Villa 0-1 Stoke
Crystal Palace 2-0 West Brom
Sunderland 2-2 West Ham
Bournemouth 1-1 Watford
Norwich 1-2 Leceister
0 comments:
Post a Comment