728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, October 03, 2015

    SHIDA:BARCELONA YAFIA PIZJUAN,YADUNDWA 2-1 NA SEVILLA,REKODI YAWEKWA

    Sevilla,Hispania.

    FC Barcelona imeanza kuonja joto ya jiwe ya kucheza bila Lionel Messi baada ya leo jioni kukubali kichapo cha goli 2-1 toka kwa FC Sevilla katika mchezo mkali wa ligi ya La Liga uliopigwa katika dimba la Estadio Sanchez Pizjuan jijini Sevilla.

    Sevilla ilianza kuonyesha mapema kuwa imechoka kuwa mteja kwa Barcelona baada ya kupata bao la kuongoza dakika ya 52 kupitia kwa Mdenmark Michael Krohn-Dehli na kisha kuongeza la pili kupitia kwa Vicente Iborra dakika ya 58 aliyepiga kichwa kizuri akiunganisha pasi ya Michael Krohn-Dehli aliyekuwa mwiba mchungu kwa walinzi wa Barcelona.

    Barcelona ilipata goli lake la kufutia machozi dakika ya 74 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Neymar Jr aliyekuwa akicheza mchezo wake wa 100 tangu ajiunge na miamba hiyo akitokea Santos ya Brazil mwaka 2013.

    Kufuatia ushindi huo Sevilla imefanikiwa kupata pointi 3 kwa mara ya kwanza tangu ilivyofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 2007 huku ikiwa imejaribu 13 bila mafanikio kuibuka na ushindi dhidi ya Barcelona.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SHIDA:BARCELONA YAFIA PIZJUAN,YADUNDWA 2-1 NA SEVILLA,REKODI YAWEKWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top