Arsenal imepata nguvu ya kumnasa winga mahiri wa kushoto wa Celta Vigo,aitwae Nolito baada ya FC Barcelona kuamua kuachana nae.
Nolito,28 aliyewahi kukipiga FC Barcelona 2008-2011 amegeuka lulu msimu huu baada ya kufanikiwa kufunga jumla ya magoli matano katika michezo sita ya La Liga huku pia akifanikiwa kupika magoli matatu.
FC Barcelona imeamua kuachana na mpango wa kumsajili Nolito kwa madai kuwa umri alionao nyota huyo kwasasa ni mkubwa hivyo huenda akawa na msaada kidogo sana.Kufuatia hatua hiyo Arsenal imejikuta ikibaki pekee yake katika mbio za kumnasa nyota huyo anayepatikana kwa dau chee la £15m.
Kazi kwenu Arsenal hiyo mwezi januari
0 comments:
Post a Comment