Madrid,Hispania.
Cristiano Ronaldo ameifungia Real Madrid mabao matano katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Espanyol katika muendelezo wa michezo ya La Liga.
Bao jingine la Real Madrid limefungwa na mshambuliaji Mfaransa Karim Benzema.Kufuatia mabao hayo matano Cristiano Ronaldo anafikisha mabao 230 katika michezo 203 na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid akimzidi nyota wa zamani wa klabu hiyo Raul Gonzalez aliyefunga mabao 228 katika michezo 550.
Katika mchezo mwingine wa La Liga FC Barcelona ilitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo mkali uliopigwa Vicente Calderon.
Atletico Madrid ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Fernarndo Torres kabla ya Nermay Jr kuisawazishia FC Barcelona na Lionel Messi kuongeza la pili akitokea benchi.
Matokeo mengine ya La Liga
• Levante 1, Sevilla 1
• Espanyol 0, Real Madrid 6
• Sporting Gijon 0, Valencia 1
• Real Betis 1, Real Sociedad 0
Michezo ya jumapili
• Granada v Villarreal
• Athletic Bilbao v Getafe
• Celta Vigo v Las Palmas
• Malaga v Eibar
0 comments:
Post a Comment