Konya,Uturuki.
Uholanzi imeendelea kujiweka katika mazingira magumu ya kufuzu katika fainali zijazo za michuano ya Euro baada ya kukubali kichapo kizito cha bao 3-0 toka kwa Uturuki.
Katika mchezo huo wa kundi A uliopigwa katika dimba la Konya wenyeji Uturuki walianza kuiadhibu Uholanzi mapema kwa kupata bao la dakika ya 8 lililofungwa na Oguzhan Ozyakup kabla ya nahodha Arda Turan kufunga la pili dakika ya 26 kisha la tatu dakika ya 85 kupitia kwa Burak Yilmaz na kuipatia ushindi wa kwanza Uturuki dhidi ya Uholanzi tangu ilipofanya hivyo mwaka 1997.
Kufuatia kichapo hicho Uholanzi imejiweka katika nafasi finyu ya kufuzu michuano ya Euro kwani imeshushwa mpaka nafasi ya nne ikiwa na alama 10 nyuma ya Czech yenye alama 19,Iceland 18 na Uturuki 12.
Msimamo ulivyo..
P W D L GD Pts
1 Czech Republic 8 6 1 1 +6 19
2 Iceland 7 6 0 1 +12 18
3 Turkey 8 3 3 2 +2 12
4 Netherlands 8 3 1 4 +3 10
5 Latvia 8 0 4 4 -12 4
6 Kazakhstan 7 0 1 6 -11 1
0 comments:
Post a Comment