Barcelona,Hispania.
Siku chache kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya kocha wa Manchester United Mdachi Louis van Gaal alitangaza kumtaka nyota wa FC Barcelona Neymar Dos Santos na kutamka kuwa yuko tayari kutoa £140m ili kumleta Mbrazil huyo Old Trafford.
Kauli hii ya Van Gaal ilionekana kama ni kichekesho kwa mashabiki wa soka duniani lakini kwa mabosi wa FC Barcelona imekuwa ni tofauti kidogo.Imekuwa kama ni kuwachongea.Wameipa uzito mkubwa kauli hiyo.Hawataki kumpoteza Neymar wala nyota wao yoyote yule anayeunda ile kombinesheni ya MSN (Messi,Suarez na Neymar)
Taarifa rasmi kutoka jiji la Barcelona zinasema FC Barcelona inajipanga kufungua mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na Neymar katika kipindi cha mapumziko ya Christmas ili kumfanya nyota huyo asifikirie kuhamia Manchester United.
Katika mkataba huo mpya wa miaka sita FC Barcelona itakuwa ikimlipa Neymar mshahara wa £500,000 kwa wiki na kuwa mchezaji anayelipwa vizuri zaidi kuliko nyota yoyote yule wa soka duniani.
0 comments:
Post a Comment