London,England.
Goli la mkwaju wa penati la dakika ya 84 limemfanya mshambuliaji Wayne Rooney awe mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya England akifikisha magoli 50 na akiivunga rekodi ya miaka 45 ya mkongwe Sir Bobby Charlton.
Rooney alifanikiwa kuivunja rekodi hiyo jana jumanne alipoisaidia England kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Uswisi katika mchezo wa kundi E wa kusaka tiketi ya kushiriki michezo ya Euro 2016 uliopigwa katika dimba la Wembley jijini London.
Goli hilo lilipatikana baada ya Raheem Sterling kudondoshwa katika eneo la hatari na mwamuzi Gianluca Rocchi kutoka Italia akaamuru upigwe mkwaju wa penati na Rooney bila kufanya ajizi alifunga kwa shuti kali na matokeo kuwa 2-0 huku goli la kwanza likifungwa na Harry Kane.
Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo...
ENGLAND:
Hart, Clyne (Stones 68), Cahill, Smalling, Shaw, Milner, Shelvey (Kane 57), Delph (Barkley 3), Oxlade-Chamberlain, Rooney, Sterling.
SWITZERLAND:
Sommer, Lichtsteiner, Klose, Schar, Rodriguez, Xhaka, Inler, Behrami (Dzemaili 79), Shaqiri, Drmic (Embolo 63), Stocker (Seferovic 72).
Matokeo mengine ya kuelekea Euro 2016
Kundi C
Hispania 1-0 Slovakia (Mata)
Slovakia 0-0 Ukraine
Kundi G
Belarus 2-0 Luxembourg (Mikhail Gordeichuk)
Austria 4-1 Sweden 4-1 (David Alaba, Marc Janko na Martin Harnik/Zlatan Ibrahimovic)
Kundi G
Urusi 7-0 Liechtenstein
Montenegro 2-0 Moldova (Stefan Savic na Petru Racu)
0 comments:
Post a Comment