728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 06, 2015

    WAJUE NYOTA WALIOSHINDWA KUHAMIA VILABU VIPYA BAADA YA KUFELI VIPIMO VYA AFYA

    Baada ya matukio ya wachezaji kufeli vipimo kuendelea kushika kasi siku hadi siku tangu utaratibu huo uanze kufanya kazi "Soka Extra" imeona ikuletee baadhi ya nyota waliowahi kushindwa kuhamia vilabu vipya baada ya afya zao kubainikia kuwa ni mgogoro.

    Remmy:Baada ya klabu ya Liverpool kumuuza mshambuliaji wake Louis Suarez kwenda klabu ya Barcelona mshambuliaji aliyepaswa kuja kuziba pengo lake alikuwa ni Mfaransa Loic Remmy ambaye kwa wakati huo alikuwa akimilikiwa na klabu ya Queens Park Rangers.Lakini kwa mshangao wa wengi nyota huyo alitangazwa kuwa amefeli vipimo vya afya katika klabu ya Liverpool kufuatia kuwa na historia ya maradhi ya moyo aliyoyapata wakati akiwa na klabu ya nyumbani kwao ya Rennes.

    Ba:Demba Ba alishindwa kuihama klabu ya Hoffenheim na kujiunga na Vfb Stuttgart baada ya vipimo kuonyesha kuwa raia huyo wa Senegal alikuwa hajapona vizuri goti lake lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu tatizo ambalo pia lilikwamisha usajili wake kwenda klabu ya Stoke City.Baadae Ba alihamia Westham kwa makubaliano ya kulipwa kutokana na idadi ya mechi ambazo angecheza.

    Fer:Klabu ya jana Agosti 5 nyota wa QPR Leroy Fer kufeli vipimo vya afya katika klabu ya Sunderland mwaka 2013 nyota huyo akiwa na FC Twente alishindwa kujiunga na Everton kwa ada ya £8.5m baada ya madaktari wa klabu hiyo ya jiji la Liverpool kugundua tatizo katika goti la nyota huyo.Baadae Everton ilikuja na ombi la kumchukua Fer na kumlipa kutokana na idadi ya mechi atakazocheza ombi ambalo lilipingwa vikali na FC Twende.

    Cissokho:Mlinzi Aly Cissokho alikosa dili la kujiunga na AC Milan baada ya miamba hiyo ya Italia kuogopeshwa na matatizo ya meno aliyokuwa nao nyota huyo.Baada ya kufanyiwa vipimo kwa mara ya pili Cissokho alifaulu vipimo lakini Milan bado ilionyesha wasiwasi kwa madai kuwa tatizo hilo lingesababisha shida katika misuli ya nyota huyo.

    Milito:Mwaka 2003 mlinzi Gabriel Milito alishindwa kujiunga na klabu ya Real Madrid baada ya daktari wa klabu hiyo Alfonso del Corro kuitaka klabu hiyo kuacha na nyota huyo kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye majeraha ya muda mrefu ya goti aliyoyapata akiwa na klabu yake ya CA Independiente Avellaneda ya Argentina kwa kuhofia kuwa tatizo hilo lingerudi tena siku za usoni.Baadae Milito alitua Barcelona na kufanikiwa kudumu kwa misimu minne.

    Marveaux:Mwaka 2011 Klabu ya Liverpool ilifuta mpango wa kumsajili winga Mfaransa Sylvain Marveaux,25 baada ya timu yake ya madaktari kusema afya ya nyota huyo ilikuwa na tatizo.Lakini masaa machache baadae Marveaux alifanyiwa vipimo vingine vya afya katika klabu ya Newcastle na kufuzu baada ya madaktari wa klabu hiyo kutoona tatizo lolote la kiafya.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAJUE NYOTA WALIOSHINDWA KUHAMIA VILABU VIPYA BAADA YA KUFELI VIPIMO VYA AFYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top