Kikosi cha ‘Wekundu wa Msimbazi’
Simba leo kitakuwa uwanjani kumenyana na timu ya Jang’ombe Boys ya
visiwani Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu ikiwa ni
sehemu ya maandalizi kwa ajili ya
msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara
inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
Kiongozi wa kambi ya Simba
visiwani humo Abul Mshangama amethibisha kuwepo kwa mtanange huo
utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni.
“Leo tunacheza saa 10 ni timu
ambayo siku za hivi karibuni imekuwa tishio na gumzo inaitwa Jang’ombe
Boys ambao siku si nyingi wameajiri kocha wao kutoka Uturuki”, amesema
Mshangama.
“Wachezaji wapo vizuri isipokuwa
Jonas Mkude bado anamajeraha na anafanya mazoezi mepesi waliobakia wote
wapo vizuri”, ameongeza.
Simba inatarajia kukamilisha
mechi zake za kirafiki visiwani Zanzibar kwa kucheza na KMKM siku ya
Jumatano na kikosi cha Simba kitarudi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
maadhimisho ya siku ya Simba Day lakini inadaiwa kuwa, kocha wa kikosi
hicho ameomba warejee tena visiwani Zanzibar mara baada ya mapumziko ya
wiki moja.
0 comments:
Post a Comment