728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 03, 2015

    SHERMAN ASAINI MIAKA MITATU MPUMALANGA,ATABIRIWA MAKUBWA

    Mpumalanga Black Aces ya Afrika Kusini imedhibitisha kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC Mliberia Kpah Sherman kwa mkataba wa miaka mitatu.

    Klabu hiyo ya AmaZayoni,Afrika Kusini kupitia kwa mwenyekiti wake Mario Morfou inaamini Sherman kwa kushirikiana vyema na mshambuliaji mkongwe wa klabu hiyo Mzambia Collins Mbesuma wataleta mafanikio makubwa.Sherman ametuma Aces kuziba pengo la Tendai Ndoro aliyetimkia Orlando Pirates.

    Akimzungumzia Sherman,Morfou amesema “Ni mchezaji mzuri na pengine ni mmoja kati ya wachezaji bora zaidi tuliowahi kuwasajili klabuni hapa.Tuna furaha kumkalibisha AmaZayoni,”

    “Atakuwa ni pacha sahihi wa Collins Mbesuma na ninaamini atakuwa ni miongoni mwa wafungaji bora katika ligi ya msimu huu.

    Sherman anakuwa ni mchezaji wa tatu kutua Afrika Kusini akitokea Tanzania baada ya Mrisho Ngassa na Uhuru Selemani.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SHERMAN ASAINI MIAKA MITATU MPUMALANGA,ATABIRIWA MAKUBWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top