Klabu ya Barcelona imemaliza mechi zake za kujiandaa na msimu mpya vibaya baada ya hapo jana jumapili kukubali kipigo cha goli 2-1 toka kwa klabu ya Fiorentina ya Italia katika mcheza mkali wa kombe la International Champions Cup uliopigwa katika dimba la Stadio Artemio Franchi.
Ikiwa bila ya nyota wake Lionel Messi na Neymar huku ikiwa ina siku tisa za kujiandaa kabla ya kuivaa klabu ya Sevilla katika mchezo wa Uefa Super Cup Barcelona ilikubali kuruhusu magoli mawili ndani ya dakika kumi na mbili za kipindi cha kwanza kwa magoli ya mshambuliaji kinda Federico Bernardeschi dakika ya 4 na 12 kabla ya Luis Suarez kuifungia goli la kufutia machozi dakika ya 16.
Barcelona inarudi Hispania ikiwa imeshinda mchezo mmoja pekee huku ikiwa imefungwa michezo mitatu tangu ilipoanza kujinoa kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Vikosi vilikuwa kama ifuatavyo....
Fiorentina: Tatarusanu; Tomovic, Gonzalo Rodriguez, Roncaglia (Bagadur 74), Pasqual (Rebic 74); Borja Valero, Badelj (Rossi 46), Joaquin (Alonso 64), Bernardeschi, Babacar (Mario Suarez 46), Ilicic (Vecino 63)
0 comments:
Post a Comment