Anaitwa Mario Balotelli.Hafanyi vizuri sana dimbani mpaka klabu yake ya Liverpool inataka kumuuza kwa bei ya hasara ili mradi tu aondoe kiwingu pale Anfield.Licha ya kuwa na kipaji kikubwa cha kusakata gozi la ng'ombe Balotelli ameshindwa kuwafanya mashabiki wa Liverpool watembee vifua mbele.Balotelli amekuwa mtu wa vituko.Balotelli huyo wa sasa siyo yule wa misimu miwili iliyopita.Balotelli huyu wa sasa kila kitu inamkana lakini kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma bado imeendelea kumuamini na hivi sasa imemtengenezea kiatu cha namna yake.
Kiatu ambacho Baloteli atakivaa msimu huu toka Puma nyuma ya kisigino kitakuwa na manyonya yanayofanana na nywele inayofanana na mtu aliyenyoa mtindo wa kiduku ambayo ndiyo unyoaji maarafu sana wa nyota huyo wa Liverpool.
0 comments:
Post a Comment