Pique akimtukana mwamuzi |
Mlinzi wa FC Barcelona Muhispania Gerard Pique huenda akakumbana na adhabu kali ya kufungiwa hadi michezo 12 ya ligi ya La Liga baada ya hapo jana jumatatu usiku kumtukana matusi ya nguoni mwamuzi msaidizi katika mchezo wa pili wa Super Cup ambapo klabu yake ya FC Barcelona ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Atletic Bilbao katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Nou Camp.
Pique akibembelezwa apunguze hasira |
Pigue alionyeshwa kadi hiyo nyekundu kwa kosa la kumvulumishia mvua ya matusi mwamuzi msaidizi baada ya kutoridhishwa na maamuzi yake.
Hii ni mara ya pili au ya tatu kwa Pique kuingia matatani kutokana na kushindwa kuzuia hisia zake awe amechukia au amefurahi.Kabla ya tukio la jana usiku,wiki iliyopita Pique aliitolea maneno makali klabu ya Real Madrid wakati akisherekea ubingwa wa EUFA Super Cup iliyoutwaa akiwa na klabu yake baada ya kuibwaga FC Sevilla kwa bao 5-4.
Kwa kawaida kitendo cha kumtolea lugha chafu mwamuzi nchini Hispania huambatana na kufungiwa kuanzia michezo minne na kuendelea hivyo kwa kuanzia Pique atakosa mchezo wa ufunguzi wa La Liga dhidi ya Athletic Club, kisha Levante,Malaga na mchezo wa Septemba dhidi ya Atletico Madrid.
0 comments:
Post a Comment