728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 18, 2015

    OLISEH AWATEMA OBI MIKEL,VICTOR MOSES KIKOSI CHA NIGERIA KITAKACHOKUJA KUIVAA STARS SEPTEMBA 5

    Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Sundey Oliseh amewatema kikosini nyota John Obi Mikel na Victor Moses katika kikosi kitakachokuja Tanzania kuivaa Taifa Stars Septemba 5 katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Africa.

    Oliseh licha ya kuwatema nyota hao wanaochezea klabu ya Chelsea ya England pia ameita kikosini nyota wengine18 wanaocheza soka nje ya Nigeria watakaoungana na wale wanaocheza ndani.

    Akizungumzia sababu ya kuwatema John Mikel Obi na Victor Moses,Oliseh amesema nyota hao wamekuwa benchi kwa kipindi kirefu hivyo haamini kama watakuwa msaada kwa Nigeria kwa kipindi hiki."Obi na Moses hawachezi mara kwa mara katika klabu yao ya Chelsea hivyo sioni sababu ya kuwatumia na kuwaacha wengine ambao wana uhakika wa kucheza kila wikendi katika vilabu vyao"Alimaliza Oliseh.

    Nigeria itaanza kambi yake Agosti 31 mjini Abuja kabla ya kuja Tanzania kuivaa Taifa Stars.

    Kikosi kama cha Nigeria kiko kama ifuatavyo.....

    Makipa: Vincent Enyeama (Lille OSC, France); Carl Ikeme (Wolverhampton Wanderers, England)

    Walinzi: Leon Balogun (FSV Mainz 05, Germany); Kingsley Madu (AS Trencin, Slovakia); Godfrey Oboabona (Caykur Rizespor, Turkey); William Troost Ekong (FK Haugesund, Norway); Kenneth Omeruo (Kasimpasa SK, Turkey)

    Viungo: Joel Obi (Torina FC, Italy); Izunna Ernest Uzochukwu (FC Amkar Perm, Russia); Obiora Nwankwo (Coimbra FC, Portugal); Lukman Haruna (Anzhi Machatsjkala, Russia); Rabiu Ibrahim (AS Trencin, Slovakia)

    Washambuliaji: Ahmed Musa (CSKA Moscow, Russia); Emem Eduok (Esperance ST, Tunisia); Emmanuel Emenike (Al Ain, UAE); Anthony Ujah (Werder Bremen, Germany); Sylvester Igboun (FC UFA, Russia); Moses Simon (KAA Gent, Belgium)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OLISEH AWATEMA OBI MIKEL,VICTOR MOSES KIKOSI CHA NIGERIA KITAKACHOKUJA KUIVAA STARS SEPTEMBA 5 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top