YANGA, Azam na Simba, zimezidi kutunishiana misuli kila moja ikitamba
kufunika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na madai ya kuwa
na kikosi bora baada ya usajili wa dirisha linalotarajiwa kufungwa
keshokutwa.
Yanga ambao ndio mabingwa wa Tanzania Bara, wamekuwa
wakijifua kwa takribani miezi miwili sasa kama ilivyokuwa kwa Azam, huku
timu hizo zikiwa zimeongeza nguvu katika vikosi vyao kwa kusajili
wachezaji wapya, wazawa na wa kigeni kama ilivyo kwa Simba.
Kati ya wachezaji wanaowapa jeuri Yanga, ni kiungo mshambuliaji mpya,
Geoffrey Mwashiuya iliyomsajili kutoka Kimondo FC ya Mbozi, Mbeya,
Malimi Busungu (Mgambo Shooting), Deus Kaseke (Mbeya City), Haji Mwinyi,
Matheo Simon na kipa Mudathir Khamis (KMKM) ambao waling’ara vilivyo na
timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika hivi karibuni
jijini Dar es Salaam na mechi kadhaa za kirafiki.
Pia wapo
wachezaji wa kigeni kama mshambuliaji,Donald Ngoma nakiungo, Thaban
Kamusoko kutoka Zimbabwe na beki wa kati, Vincent Bossou raia wa Togo.
Wachezaji hao wapya na wale wa zamani kama viungo Haruna Niyonzima,
Salum Telela, Ally Mustapha ‘Barthez’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin
Yondani, Andrey Coutinho, Simon Msuva na wengineo ndio wanaoonekana
kumpa jeuri Kocha Mkuu wao, Mholanzi Hans van der Pluijm ambaye ameweka
wazi kuwa msimu ujao ni wao.
0 comments:
Post a Comment