728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 01, 2015

    HII HAPA SABABU ILIYOFANYA SERIKALI IKATAE KUMLIPA MKWASA MSHAHARA WA KUINOA TAIFA STARS


    Serikali imekataa kumlipa mshahara kocha wa muda wa Taif Stars, Charles Mkwasa kwa kisingizio kuwa fedha hizo ni maalum kwa wageni tu, tofauti maombi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

    Wakati TFF ikimpa kazi Mkwas ya kuinoa Taifa Stars, rais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi alisema angeiomba serikali iml kocha huyo stahiki zote kama ilivyokuwa ikifanya kwa makoch wageni.

    Taarifa zimeeleza Serikali imegoma kumlipa Mkwasa na bada yake TFF imekuwa ikimlipa posh kocha huyo kama kifuta jasho.

    Alipotafutwa Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa kutoa ufafanuzi wa sakata hilo, alisema: “Ni kweli hakuna mali ya mshahara wa Mkwasa yaliyofanywa na serikali, ila sisi kama TFF tulimlipa posho kwa kazi yake. Tupeni muda tunalifanyia kazi jambo hili.”

    Kuhusiana na malipo ya aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars Mart Nooij ambaye bado yupo nchini, Mwesigwa alisema: “Noo hatudai chochote, tumeshamaliz naye na kama yupo nchini ni kw mapenzi yake tu.”

    Hivi karibuni TFF katika maazimio ya kamati yake ya utendaji ilikubaliana kusitish mkataba wa Nooij na nafasi yak kupewa Mkwasa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HII HAPA SABABU ILIYOFANYA SERIKALI IKATAE KUMLIPA MKWASA MSHAHARA WA KUINOA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top