Manchester, England.
Chelsea imekubali kipigo cha kwanza cha msimu mpya wa ligi kuu baada ya kukubali kichapo cha goli 3-0 toka kwa Manchester City katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Etihad jijini Manchester.
Goli la kwanza la Manchester City limefungwa na mshambuliaji Sergio Aguero (36) baada ya kugongeana vyema na kiungo Yaya Toure na kisha kuwalamba chenga walinzi wa Chelsea na kumfunga kirahisi mlinda mlango Asmir Begovic.
Goli la pili la Manchester City limefungwa na nahodha Vincent Kompany (79) kwa kichwa akiunganisha kona iliyopigwa na kiungo David Silva huku kiungo Fernandinho akifunga goli la tatu (85).
0 comments:
Post a Comment