Cavani:Arsenal imeripotiwa kuandaa kitita cha £35.5m ili kumsajili mshambuliaji wa PSG Edinson Cavani baada ya kuachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema.(Metro)
Stones:Chelsea ina hofu kuwa Manchester United
na Manchester City zinamtaka kwa siri mlinzi wa Everton John Stones hivyo kufanya mbio za kumnasa mlinzi huyo kuwa ngumu.(Mail on Sunday)
Malouda:Winga wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Metz Mfaransa Florent Malouda huenda akajiunga na Delhi Dynamos ya India baada ya leo kutua katika jiji la New Delhi kukamilisha uhamisho huo.
Berahino:Sasa Tottenham Hotspur iko tayari kuongeza pesa mpaka kufikia £20m ili kuipata saini ya mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino.(Sunday Mirror)
Zouma:Kocha wa AS Roma Rudi Garcia ameandaa kitita cha £25m ili kumsajili mlinzi wa Chelsea Kurt Zouma ili kuziba nafasi ya mlinzi Alessio Romagnoli aliyejiunga na AC Milan wiki iliyopita.
Benitez:Kocha wa Real Madrid Rafael Benitez anapanga kukiongezea nguvu kikosi chake kwa kuwasajili nyota wawili wanaotesa Seria A Lucas Biglia,29 na Fernando Llorente,30.(Marca)
Mori:Everton iko tayari kutoa £8m kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa River Plate Ramiro Funes Mori ili kuchukua nafasi ya mlinzi John Stones anayewindwa na Chelsea.(Sunday Express)
Kurzawa:Liverpool na Tottenham wanakaribia kuikosa saini ya mlinzi wa kushoto wa Monaco Layvin Kurzawa,baada ya nyota huyo kupendelea kutua Paris Saint-Germain.(Sunday People)
0 comments:
Post a Comment