Klabu ya Yanga SC leo jioni imeibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya klabu ya Mbeya City katika mchezo mkali wa kirafiki uliopigwa katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Yanga ambayo ilitua Mbeya wiki iliyopita kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam FC ilipata magoli yake kupitia kwa Andre Coutinho (16),Hamisi Tambwe (45) na Donald Ngoma (47) huku yale ya Mbeya City yakifungwa na Bakari Mwinjuma (8) pamoja na Meshack Ilemi (83).
Katika mchezo huo Yanga iliwachezesha nyota wake wapya Thabani Kamusoko na Vincent Bossou
0 comments:
Post a Comment