728x90 AdSpace

Monday, January 12, 2015

JUVE YAINYUKA NAPOLI 3-1,ROMA YAISHINDWA LAZIO


Napoli, Italia.
Magoli mawili ya viungo Paul Pogba na Athuro Vidal na mlinzi Martin Cacerez yalitosha kuipa klabu ya Juventus ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya klabu ya Napoli iliyopata goli lake kupitia kwa mlinzi Miquel Britos  katika dimba la Stadio San Paolo mjini Naples jana usiku.


Ushindi huo ni wa kwanza kwa Juventus kupata nyumbani kwa Napoli katika kipindi cha miaka 15 tangu ilipofanya hivyo mwaka 2000. Kufuatia ushindi huo Juventus imeendelea kung'ang'ania katika usukani wa ligi ya Seria A ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 43 baada ya kushuka dimbani mara 18 nafasi ya pili inashikiliwa na Roma yenye pointi 40

Matokeo mengine ya Seria A
Inter Milan 3-1 Genoa
Atalanta1 - 1 ChievoVerona
Cagliari  2 - 1 Cesena
Fiorentina  4 - 3 Palermo
Hellas Verona 3 - 1 Parma
Roma 2 - 2 Lazio
Sampdoria 1 - 0 Empoli
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: JUVE YAINYUKA NAPOLI 3-1,ROMA YAISHINDWA LAZIO Rating: 5 Reviewed By: Unknown