KIUNGO wa Chelsea Mfaransa,N'Golo Kante ameendelea kuwa na msimu mzuri na wenye mafanikio baada ya usiku wa kuamkia leo kutangazwa mshindi wa tuzo ya tuzo ya waandishi wa habari za michezo maarufu kama Football Writers' Player of the Year (FWA).
Kante ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Eden Hazard aliyeshika nafasi ya pili na Dele Alli aliyeshika nafasi ya tatu.Ikumbukwe kuwa Kante ndiye mshindi pia wa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu PFA kwa msimu wa 2016/17 hivyo anakuwa mchezaji wa 20 kutwaa tuzo mbili katika msimu mmoja.BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI
0 comments:
Post a Comment