Johanesburg,Afrika Kusini.
Bidvest Wits ama The Clever Boys ndiyo mabingwa wapya wa ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini maarufu kama PSL kwa msimu wa 2016/17 kufuatia ushindi wao wa mabao 2-0 walioupata nyumbani Bidvest Stadium dhidi ya wageni wao Polokwane City.
Mabao yaliyoandikisha ubingwa huo wa kwanza kwa timu hiyo yamefungwa na James Keene na Daine Klate na kuwaacha kwenye mataa wabingwa wa msimu uliopita Mamelodi Sundowns kwa tofauti ya pointi sita.
Bidvest Wits inakuwa timu ya saba kutwaa ubingwa wa PSL huku kocha wake,Gavin Hunt akiwa ubingwa huo kwa mara ya nne.Mara tatu akiwa na SuperSport United msimu wa 2007/08, 2008/09 na 2009/10.
Matokeo Mengine ya Mei 17
Bidvest Wits 2-0 Polokwane City
Mamelodi Sundowns 2-2 Maritzburg United
Chippa United 3-0 SuperSport United
Platinum Stars 2-0 Kaizer Chiefs
Orlando Pirates 0-0 Ajax Cape Town
Cape Town City 1-0 Golden Arrows
Baroka FC 0-0 Highlands Park
Bloemfontein Celtic 0-0 Free State Stars
Ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini itafikia tamati Jumamosi Mei 27.
0 comments:
Post a Comment