728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 10, 2017

    Ligi kuu bara:Simba yawaua Mbao FC dakika za lala salama,Azam,Mtibwa zashindwa kutambiana


    Farid Miraji,Dar Es Salaam.
    Timu ya Simba imetokea kufungwa mabao mawili nyuma na  kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa katika dimba la CCM Kirumba leo jioni.


    Wenyeji Mbao walipata bao la  kuongoza kupitia kwa George Sanguja dakia ya 20 aliyefunga kwa shuti kali kutokea upande wa kulia.

    Bernard Evaristu akaipeleka mbele zaidi Mbao kwa bao la pili kabla ya kipindi cha kukatika pale alipowazidi maarifa walinzi wa Simba waliojichanganya na kumruhusu kuzitikisa nyavu za Manyika.

    Kocha Joseph alilazimika kufanya mabadiliko kadhaa ambayo yalikuja kuzaa matunda kipindi cha pili kwa Fredrick Blagnon aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Juma Liuzio.
    Blagnon aliyerejea hivi karibuni akitokea Oman alifunga mabao hayo dakika ya 82 na 91 na kisha Yassin Mzamiru akafunga bao la ushindi katika dakika ya mwisho ya muda wa majeruhi.
    Kwa ushindi huo Simba inarudi kileleni kwa kuipindua Yanga kwa tofauti ya pointi mbili japo wapinzani wao wana mchezo mmoja mkononi.

    Katika mchezo mwingine wa ligi kuu bara uliochezwa leo jioni Azam FC imetoshana nguvu na Mtibwa Sugar baada ya kutoka sare ya bila kufungana huko Manungu Complex.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ligi kuu bara:Simba yawaua Mbao FC dakika za lala salama,Azam,Mtibwa zashindwa kutambiana Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top