728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 10, 2017

    Aubameyang ni wa Barcelona na Real Madrid wengine mnajisumbua tu


    Dortmund,Ujerumani.

    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Gabon,Pierre-Emerick Aubameyang hatajiunga na vilabu vingine vya barani Ulaya katika dirisha lijalo la usajili zaidi ya Real Madrid na Barcelona.Hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa klabu yake ya Borussia Dortmund,Hans-Joachim Watzke.

    Watzke ametoa kauli hiyo baada ya hivi karibuni Aubameyang mwenye umri wa miaka 27 kuripotiwa kuwa kwenye mawindo ya vilabu mbalimbali vikubwa barani humo vikiwemo vilabu tajiri vya nchini England vya Manchester City,Liverpool na Arsenal. 

    Watzke anaamini kuwa Real Madrid na Barcelona ndivyo vilabu pekee vyenye hadhi ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Saint Etienne ya Ufaransa na kusisitiza kuwa angependa kumwona Aubameyang akijiunga navyo siku moja.

    Aidha Watze ameongeza kuwa mshambuliaji huyo anayekadiriwa kuwa na thamani ya £100m hata iweje hatauzwa kwenda kwa mahasimu wao wakubwa wa Bundesliga,Bayern Munich kama ilivyokuwa kwa Wajerumani Mario Gotze na Mats Hummels waliouzwa kwenda Allianz Arena katika vipindi viwili tofauti. Aubameyang bado ana mkataba na Borussia Dortmund mpaka mwaka 2020.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Aubameyang ni wa Barcelona na Real Madrid wengine mnajisumbua tu Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top