728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 12, 2017

    Robo fainali ya kwanza Ulaya:Juventus yaitoa nishai Barcelona,yainyuka 3-0


    Turin,Italia.

    JUVENTUS imejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya usiku wa leo kuifunga Barcelona kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Juventus Arena uliopo jijini Turin.

    Paul Dybala ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo wa leo baada ya kuifungia Juventus mabao mawili ya kipindi cha kwanza ya dakika za 7 na 22 akimalizia kazi safi za Juan Cuadrado na Mario Mandzukic.Bao la tatu la Juventus limefungwa kwa kichwa na mlinzi Giorgio Chiellini katika dakika ya 55 akiunganisha kona ya Miralem Pjanic.



    Aidha katika mchezo huo ilishubudiwa Barcelona ikishindwa kutengeneza nafasi za kutosha za kufunga mabao licha ya kuwa na umiliki mkubwa wa mpira.

    Timu hizo zitarudiana tena Aprili 19 mwaka huu na timu itakayokuwa na ushindi mkubwa wa jumla ndiyo itakayofuzu hatua ya nusu fainali.

    Vikosi Vilikuwa

    Juventus: Buffon; Alves, Bonucci, Chiellini,Alex Sandro; Khedira, Pjanic (Barzagli 89);Cuadrado (Lemina 73), Dybala (Rincon 81),Mandzukic; Higuain

    Barcelona: Ter Stegen; Pique, Umtiti, Mathieu (Gomes 46); Sergi, Rakitic, Mascherano,Iniesta; Messi, Suarez, Neymar

    Mwamuzi:Marciniak (POL)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Robo fainali ya kwanza Ulaya:Juventus yaitoa nishai Barcelona,yainyuka 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top