728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, April 11, 2017

    Bayern yamshangaa beki wake kuukataa Ukurugenzi


    Munich,Ujerumani.

    WAKATI tatizo la ukosefu wa ajira likiripotiwa kuendelea kushika kasi karibu kila pande ya dunia hii huku wake kwa waume kutwa nzima wakiwa viguu na njia kusaka sehemu za kupatia mkate wa siku imebainika kuwa kumbe wapo wanaopewa ajira hata bila ya kuzitolea jasho lolote kama wengine na bado wanazikataa.

    Ishu iko hivi beki na nahodha wa Bayern Munich,Philipp Lahm amekikataa cheo cha Ukurugenzi wa Michezo (Sporting Director) alichoahidiwa kupewa na klabu yake hiyo pindi atakapostaafu kucheza mpira mwishoni mwa msimu huu.

    Hilo limefichuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo,Karl-Heinz Rummenigge wakati akifanya mahojiano na jarida la michezo la Ujerumani la PDA.

    Rummenigge amekiri kuwa walikuwa kwenye mazungumzo na Lahm,33, juu ya kukitwaa cheo hicho kilichokuwa wazi tangu Agosti mwaka jana baada ya aliyekuwa akikishikilia Matthias Sammer kujiuzulu lakini nyota huyo anayecheza nafasi nyingi uwanjani amekataa.


    "Kulikuwa na uvumi mwingi kuhusu jambo hili.Ni kweli tulikuwa kwenye mazungumzo ya awali na Lahm na tulipenda achukue nafasi ya Sammer lakini cha ajabu ameikataa ofa yetu.Tunaheshimu uwamuzi wake.Bado milango iko wazi kwake katika siku za usoni.

    Mbali ya Lahm mwingine aliyedaiwa kukikataa cheo hicho ni Mkurugenzi wa Michezo wa sasa wa Borussia Monchengladbach,Max Eberl 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Bayern yamshangaa beki wake kuukataa Ukurugenzi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top