Moroni,Comoro.
MABINGWA wa Tanzania,Yanga SC leo Jumapili mishale ya saa 9:00 za mchana watashuka katika dimba la ugenini la Stade de Moroni (ICR) huko Moroni - Ngazidja,Comoro kuvaana na wenyeji wao Ngaya De Mbe kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua ya awali ya michuano ya klabu bingwa Afrika.
Katika mchezo wa leo Yanga SC itawakosa nyota wake watatu wa kutumainiwa Vincent Bossou,Donald Ngoma na Andre Vincent 'Dante' wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kadi na majeruhi.
Ikiwa Yanga SC itafanikiwa kuing'oa Ngaya De Mbe itacheza na mshindi kati ya Zanaco FC ya Zambia au APR ya Rwanda ambao katika mchezo wao wa jana walitoshana nguvu kwa kutoka sare ya 0-0.
Ratiba ya leo Jumapili
Ngaya Club (Com) v Young Africans (Tan)
Wa All Stars (Gha) v Al Ahly Tripoli (Lib)
Cotonsport (Cmr) v Atlabara (Ssu)
Leopard (Con) v UMS de Loum (Cmr)
Barrack Young Controllers (Lib) v Stade Malien (Mli)
Gambia Ports (Gam) v Sewe (Ivo)
Ela Nguema (Gnq) v Al-Merreikh (Sud)
Matokeo ya michezo ya Jumamosi
Real Bamako (Mli) 0 - 0 Rivers United FC (Nig)
US Goree (Sen) 0 - 0 Horoya (Gui)
Kadiogo (Bur) 3 - 0 Diables Noirs (Con)
Tanda (Ivo) 3 - 0 ASFAN (Nig)
Saint-Louisienne (Reu) 2 - 1 Bidvest Wits (Rsa)
FC Johansen (Sie) 1 - 1 FUS Rabat (Mar)
CF Mounana (Gab) 2 - 0 Vital'O (Bur)
Lioli (Les) 0 - 0 CAPS Utd (Zim)
Zimamoto (Zanz) 2 - 1 Ferroviario Beira (Moz)
Zanaco (Zam) 0 - 0 APR (Rwa)
0 comments:
Post a Comment