London,England.
MWAMUZI Mark Clattenburg amewaomba radhi wachezaji wa Hull City kufuatia kulikubali kimakosa goli la mkono la mkono la Alexis Sanchez lililoipa Arsenal ushindi wa mabao 2-0 jana Jumamosi nyumbani Emirates.
Mlinzi wa Hull City,Andrew Robertson amesema Clattenburg aliwafuata wakati wa mapumziko na kuwaomba radhi na kukiri kuwa kweli goli hilo lilikuwa ni la mkono.
Robertson ameongeza kuwa Clattenburg alishindwa kulikataa bao hilo mara moja kwa kuwa hakuwa na uhakika kwa asilimia mia moja.
Wakati huohuo wachezaji wa Hull City wamemshutumu Clattenburg kwa kushindwa kumtoa uwanjani mlinzi wa Arsenal Kieran Gibbs baada ya kumchezea madhambi winga Lazar Markovic.
0 comments:
Post a Comment