Corinthians, Brazil
TIMU ya taifa ya Nigeria ya vijana waliochini ya miaka 23 imeshindwa kufuzu fainali ya olimpiki kwa upande wa soka la wanaume baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 toka kwa vijana wenzao wa Ujerumani katika mchezo mkali wa nusu fainali uliochezwa Jumatano Usiku katika Uwanja wa Arena Corinthias.
Mabao ya washindi Ujerumani yamefungwa na Lukas Klostermann dakika ya 9 pamoja na Nils
Petersen dakika ya 89.
Kwa matokeo hayo sasa Ujerumani itavaana na wenyeji Brazil katika mchezo wa fainali wa kuwania medali ya dhahabu huku Nigeria ikivaana na Honduras kusaka medali ya shaba.
0 comments:
Post a Comment