Barcelona,Hispania.
BARCELONA imetwaa taji la Supercopa de Espana Jumatano Usiku baada ya kuifunga Sevilla kwa mabao 3-0 katika mchezo wa mkondo wa pili uliochezwa katika uwanja wa Camp Nou,Barcelona.
Mabao ya Barcelona yamefungwa na Arda Turan aliyefunga mara mbili dakika za 10 na 46' bao la tatu limefungwa na Lionel Messi dakika ya 55.
Kwa matokeo hayo Barcelona imeibuka mshindi kwa jumla ya mabao 5-0 kufuatia katika mchezo wa awali uliochezwa huko Ramon Sanchez Pizjuan siku ya Jumapili kushinda kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Luis Suarez pamoja na Munir El Haddadi.
Taji la Supercopa de Espana huwa ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa msimu mpya wa ligi ya La Liga.Humkutanisha bingwa wa La Liga na bingwa wa Kombe la Copa de Rey.
0 comments:
Post a Comment