Napoli,Italia.
NAPOLI imemsajili Mshambuliaji wa Poland,Arkadiusz Milik,kutoka Ajax ya Uholanzi kwa dau la €34m ambalo limevunja rekodi ya usajili nchini humo.
Milik,22,amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea Napoli hii ni baada ya kufaulu vipimo vyake vya afya na atakuwa akivalia jezi Namba 99 katika kipindi chote atakachokuwa akiitumikia klabu hiyo ya Stadio San Paolo.
Napoli imemsajili,Milik,ili kuja kuchukua nafasi ya Mshambuliaji wake wa zamani,Gonzalo Higuain,aliyehamia Juventus kwa dau la €90m ambalo limeweka rekodi ya usajili nchini Italia.
Milik alijiunga na Ajax mwaka 2015 akitokea Bayer Leverkusen kwa dau dogo la €2.8m.Kabla ya hapo aliichezea Ajax kwa mkopo wa msimu mmoja.
Katika msimu wake wa kwanza (2014/14) akiwa na Ajax kwa mkopo,Milik,alifanikiwa kufunga mabao 23 na kutengeneza mengine kumi na moja katika michezo 33.
Katika msimu wake wa pili ambao umeisha mwezi Mei (2015/16),Milik,alifunga mabao 24 katika michezo 42 huku pia akihusika katika kutengeneza mabao mengine manane.
Milik ameifungia Poland mabao 11 na alikuwa sehemu ya kikosi hicho kilichofika hatua ya robo fainali ya michuano ya Euro 2016 iliyofikia tamati mwezi Juni nchini Ufaransa.
Kabla ya kumnasa,Milik,Napoli ilikuwa tayari imeshawanasa nyota wawili ambao ni beki Lorenzo Tonelli kutoka Empoli na kiungo Emanuele Giaccherini kutoka Sunderland.l
0 comments:
Post a Comment