Manchester,England.
Klabu ya Manchester City imeendelea na ujenzi wa kikosi chake kipya chini ya kocha wake Mhispania,Pep Guardiolabaadda ya hivi punde kufanikiwa kumnyakuwa winga,Leroy Sane,kutoka Schalke 04 ya Ujerumani kwa ada ya £37m.
Sane,20,amesaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka katika jiji la Manchester mpaka mwaka 2021 na atakuwa akivalia jezi namba 19.
Akiongea na mtandao wa klabu hiyo,ManCity.com,Sane,ameelezea furaha yake baada ya uhamisho huo kukamilika pia amemsifia Kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola kuwa ndiye aliyemshawishi kwa kiasi kikubwa mpaka akakubali kuachana na Shalke 04.
Msimu uliopita,Sane, aliichezea Shalke 04 jumla ya michezo 42 na kuifungia mabao manane na kufanikiwa kupika mengine (assists) sita.
Sane anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na Manchester City baada ya Manuel Arago Nolito,Ilkay Gundogan, Aaron Mooy na Oleksandr Zinchenko.
0 comments:
Post a Comment