728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 15, 2016

    LIGI YA MABINGWA AFRIKA: WYDAD,ZESCO ZAFUZU NUSU FAINALI,AL AHLY ,ASEC OUT,


    Rabat,Morocco.

    WAYCasablanca name nca ya Morocco imeungana na Zesco United ya Zambia kufuzu nusu fainali ya michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika baada ya Jumapili Usiku kuibuka na Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo Mkali wa kundi A uliochezwa huko Rabat,Morocco.

    Mabao ya washindi Wydad Casablanca yamefungwa na Abdeladim Khadrouf pamoja na Fabrice Ondama huku lile la ASEC Mimosas likifungwa na Yannick Zakri.

    Matokeo hayo yameifanya Wydad Casablanca iendelee kukalia kiti cha uongozi wa kundi A baada ya kufikisha alama 10.Zesco United ni ya pili na alama zake nane.Al Ahly ni ya tatu ikiwa na alama tano ikifuatiwa na ASEC Mimosas yenye alama nne.

    Kwa maana hiyo Wydad Cassablanca na Zesco United zimefuzu nusu fainali huku Al Ahly na Asec Mimosas zikifungishwa virago licha ya kubakiwa na mchezo mmoja mmoja mkononi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI YA MABINGWA AFRIKA: WYDAD,ZESCO ZAFUZU NUSU FAINALI,AL AHLY ,ASEC OUT, Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top