Jasper Cillessen
Fabinho:Baada ya kumpata Antony Martial msimu uliopita,Manchester United,imepania tena kurudi Monaco kwa ajili ya kumsajili beki wa kulia wa klabu hiyo Fabinho,22,anayepatikana kwa ada ya £25m.(Marca/Mirror)
Rodriguez:Chelsea inaangalia uwezekano wa kukipanua kikosi chake kwa kumsajili beki wa kushoto wa VFL Wolfsburg,Ricardo Rodriguez mwenye thamani ya £22m ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na mabeki Baba Rahman na Papy Djilobodji waliojiunga na vilabu vya Shalke na Sunderland.(Daily Mirror )
Eduardo:Meneja wa Dinamo Zagreb ya Croatia,Zlatko
Kranjcar,amefichua kuwa mlinda mlango mkongwe wa klabu hiyo Eduardo,33,atahamia Chelsea Agosti 24 mwaka huu baada ya kuichezea klabu hiyo katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Red Bull Salzburg ya Austria.(The Sun)
Wenger:Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger,ameripotiwa kuwa atawasajili mabeki Fabian Schar wa Hoffenheim ama Marcel Tisserand wa Monaco ikiwa atashindwa kumsajili beki wa Valencia,Shkodran Mustafi.(France Football)
Luan: Rennes ya Ufaransa imeungana na vilabu vya Liverpool na Leicester katika mbio za kutaka kumsajili mshambuluaji kinda wa Gremio na Brazil,Luan,20.(RMC)
Remy:Crystal Palace imevutiwa na mpango wa kutaka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea,Loic Remy,baada ya kupata ugumu katika mbio zake za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool,Christian Benteke.(L'Equipe)
Cillessen:Barcelona imefungua mazungumzo na Ajax kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kumsajili mlinda mlango wake,Jasper Cillessen,27,mwenye thamani ya €12m.Barcelona imeamua kumgeukia Cillessen baada ya kuwa katika hatari ya kumpoteza mlinda mlango wake Claudio Bravo anayewindwa na Manchester City.(Mundo Deportivo)
0 comments:
Post a Comment