Zagreb, Croatia.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania,Mbwana Samatta,amefunga bao moja na kuiwezesha klabu yake ya KRC Genk kupata sare ya kufungana mabao 2-2 na klabu ya Lokomotiva Zagreb katika mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kuingia katika hatua ya makundi ya michuano ya Europa Ligi.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Stadion Kranjcevicenca,Genk ndiyo waliokuwa wa kwanza kuliona lango wa wenyeji wao Lokomotiva Zagreb baada ya kupata mabao kupitia kwa Leon Bailey 35' na Mbwana Samatta 47' ambaye baadae alitoka na nafasi yake ikachukuliwa na Nikos Karelis.
Kuingia kwa mabao hayo kuliwaamsha Lokomotiva Zagreb ambao walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha mabao hayo kupitia kwa 51 Mirko Marić 52 na Ivan Fiolic 58'.
Timu hizo zitarudiana tena siku ya Alhamisi huko Genk,Ubelgiji na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi ya michuano ya Europa Ligi.
Vikosi
Lokomotiva (4-2-3-1): Zagorac - Bartolec,Majsotorović, Perić, Rožman - Šunjić, Ćorić -Grezda, Fiolić, Bočkaj - Marić.
Genk (4-2-3-1): Bizot - Walsh, Dewaest,Colley, Uronen - Heynen, Ndidi - Buffel,Pozuelo, Bailey,Samatta
0 comments:
Post a Comment