Mavugo
Dar Es Salaam,Tanzania.
JANA Ijumaa jioni klabu ya Simba SC ikiongozwa na Rais wake,Evans Aveva,ilifunga usajili kwa wachezaji wa kigeni (Mapro) baada ya kuwasainisha mikataba nyota watano kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.
Bokungu
Nyota hao waliosainishwa mikataba ni Washambuliaji,Laudit Mavugo (Burundi),Fredrick Blagnon (Ivory Coast),Walinzi Jonvier Bokungu (DRC),Method Mwanjale (Zimbabwe) na kiungo Mussa Ndusha (DRC).
Mwanjale
Nyota hao wanaungana na nyota wengine wawili waliokuwepo klabuni hapo Mlinzi Juuko Murshid na Mlinda Mlango Agban na kufanya Simba ifikishe wachezaji saba wa kigeni ambayo ndiyo idadi ya mwisho kwa mujibu wa sheria za shirikisho la soka nchini TFF.
Ndusha