Sunderland,England.
MLINZI wa kati wa kimataifa wa Senegal,Papy Djilobodji,amejiunga na Sunderland akitokea Chelsea kwa ada ya uhamisho ya £8m.
Djilobodji,27,amesaini kandarasi ya miaka minne kuichezea Sunderland baada ya kufuzu vipimo vya afya na anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa klabu hiyo,David Moyes.
Djilobodji alijiunga na Chelsea mwezi Agosti mwaka jana akitokea Nantes ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho ya £2.7m lakini alijikuta akisota benchi kwa kipindi cha miezi sita baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.
Katika kipindi chote cha miezi sita alichokuwa na Chelsea,Djilobodji,alifanikiwa kucheza mchezo mmoja tu tena hii ilikuwa katika michuano ya Capital One ambapo Chelsea iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Walsall.
Januari 2016,Djilobodji, alijiunga na Werder Bremen ya Ujerumani kwa mkopo wa msimu mmoja na kuinusuru klabu hiyo kushuka daraja baada ya kufunga bao la kichwa lililoipa Werder Bremen ushindi wa bao 1-0 dhidi Eintracht Frankfurt katika mchezo wa mwisho wa ligi ya Bundesliga.
Djilobodji alianza safari yake ya kucheza mpira akiwa na klabu ya nyumbani kwao ya ASC Saloum kabla ya mwaka 2010 kujiunga na Nantes akitokea klabu ndogo ya US Senart Moissy ya Ufaransa.
Akiwa na Nantes,Djilobodji,alifanikiwa kuichezea klabu hiyo zaidi ya michezo 150 hali iliyofanya Chelsea kumgeukia kama suluhisho la haraka baada ya kushindwa kumnasa mlinzi wa Everton,John Stones.
0 comments:
Post a Comment