Swansea,Wales.
Swansea City imekiongezea makali kikosi chake tayari kwa msimu ujao wa ligi kuu nchini England hii ni baada ya kumsajili mshambuliaji Fernando Llorente kutoka Sevilla kwa ada ya uhamisho ya $8.6m.
Llorente,31,mshindi wa kombe la dunia mwaka 2010 na Euro 2014 akiwa na Hispania amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Swansea City na atakuwa akivaa jezi Namba 9 katika kipindi chote atakachokuwa akiitumikia miamba hiyo ya Wales.
Swansea City imemsajili Llorente ili kuja kuchukua nafasi za washambuliaji Alberto Paloschi, Bafetimbi Gomis na Elder walioihama klabu hiyo katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.
Kabla ya kutua Swansea City,Llorente,aliwahi kuvichezea vilabu vya Athletic Bilbao ya nyumbani kwao Hispania na Juventus ya Italia.
0 comments:
Post a Comment