728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 06, 2016

    MANJI APEWA YANGA KWA MIAKA KUMI

    Dar Es Salaam,Tanzania.

    WANACHAMA wa Yanga wamekubali kumkodisha klabu hiyo Mwenyekiti wao,Yusuf Manji kwa miaka 10 kuanzia leo.

    Uamuzi huo umefikiwa katika Mkutano Mkuu wa dharula uliofanyika leo ukumbi wa Diamond jubilee, Dar es Salaam.

    Manji ameomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.

    Na katika kipindi hicho cha miaka 10, timu ya soka na nembo ya klabu zote zitakuwa chini ya Manji.

    Aidha, Mjumbe wa Baraza
    la Wadhamini la klabu,Francis Kifukwe alisema baada ya wanachama kuridhia mpango huo, wao wanampa pia ridhaa hiyo Manji.

    Mkutano wa Yanga unaendelea hivi sasa Diamond Jubilee na awali wanachama watatu wa klabu hiyo, Ayoub Nyenzi, Salum Mkemi na Hashim Abdallah walifukuzwa.

    Manji aliwaambia wanachama hayuko tayari kufanya kazi na Wajumbe hao wa Kamati yaUtendaji na akaomba wanachama wanaowataka wajitokeze
    kupiga kura, lakini hakuna aliyeinuka.

    Baada ya kurudia kuita mara tatu, Hashim pekee kati ya watatu hao ambaye alikuwepo mkutanoni
    ukumbi wa Diamond Jubilee, akainuka na kuondoka.

    Mwanachama mwingine,Siza Lyimo ambaye Manji alitaka aondoke, yeye
    aliomba msamaha na wanachama wakamsamehe na Mwenyekiti huyo akabariki msamaha huo.

    Mkemi na Nyenzi hawakutokea kwenye Mkutano huo.

    (CHANZO:BIN ZUBERY)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MANJI APEWA YANGA KWA MIAKA KUMI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top