728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 07, 2016

    KIRAFIKI:AZAM FC YABANWA MBAVU NA RUVU SHOOTING

    Mlandizi,Pwani.

    AZAM FC imebanwa mbavu na Ruvu Shooting baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo mkali wa kirafiki uliochezwa katika Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi,Pwani.

    Ruvu Shooting ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao baada ya Shaban Kisiga kufunga kwa mkwaju wa faulo dakika ya 13 ya mchezo.

    Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Azam FC ambayo ilikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 44 kupitia kwa Muivory Coast,Ibrahima Fofana.

    Fofana alifunga bao hilo baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Ruvu Shooting na kufanya mchezo huo uishe kwa sare ya bao 1-1.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIRAFIKI:AZAM FC YABANWA MBAVU NA RUVU SHOOTING Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top