Ufaransa.
IKICHEZA soka la kuvutia na la ufundi wa hali ya juu, timu ya taifa ya Ufaransa,imetinga nusu fainali ya michuano ya Euro 2016 baada ya usiku huu kuifumua Iceland kwa mabao 5-2 katika mchezo mkali wa robo fainali uliochezwa katika uwanja wa Stade de France,Paris.
Mpaka mapumziko, Ufaransa ilikuwa kifua mbele kwa mabao manne ya Olivier Giroud,Paulo Pogba,Dimitri Payet na Antoine Griezman.
Mwanzoni mwa Kipindi cha pili,Olivier Giroud aliifungia Ufaransa bao la tano kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Dimitri Payet.Mabao ya Iceland yamefungwa na Kolbeinn Sigthórsson pamoja na Birkir Bjarnason.
Kwa kushinda mchezo huo,Ufaransa sasa itavaana na Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali utakaochezwa Alhamis.Hii ni nusu fainali yake ya kwanza tangu mwaka 2000.
Ujerumani ilitinga nusu fainali baada ya kuifunga Italia kwa penati 6-5 kufuatia sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 120.
0 comments:
Post a Comment