Swansea,Wales.
HAPA KAZI TU!!Wakati leo ikiwa ni siku ya mapumziko katika sehemu kubwa ya dunia kupisha maadhimisho ya sikukuu ya Eid,vilabu vya Swansea City na West Bromwich Albino vyenyewe vimekuwa bize kuimarisha vikosi vyao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu England.
Swansea City imemsajili beki wa kati wa Uholanzi,Mike van der Hoorn kutoka Ajax kwa ada ya £2m.
Hoorn,23,amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia miamba hiyo ya Liberty Stadium na mtihani wake mkubwa utakuwa ni kupata namba kikosi cha kwanza mbele ya nahodha Ashley Williams, Federico Fernandez na Jordi Amat.
Hoorn anakuwa mchezaji wa pili toka Uholanzi kujiunga na Swansea City ndani ya masaa yasiyozidi 48.Wa kwanza alikuwa na Leroy Fer aliyejiunga na Swansea City jana akitokea QPR kwa ada ya £4.1m.
WESTBROM
West Brom imetangaza kumsajili mshambuliaji wa Scotland,Matt Phillips kutoka Queens Park Rangers kwa ada ya £5m.
Phillips,25,amesaini mkataba wa miaka minne na tayari ameishajiunga na kikosi hicho tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu England.
0 comments:
Post a Comment