Tiemoue Bakayoko
Samatta:Wakala wa Mbwana Samatta,Jamal Kisongo,amesema mteja wake anahitaji msimu mmoja zaidi wa kuendelea kuichezea KRC Genk ili aweze kuongeza uzoefu wa kucheza Ulaya pamoja na kuongeza thamani yake kabla ya kufikiria ofa zilizoletwa mezani na vilabu toka Urusi na Uturuki.(Radio One)
Lacazette:Arsenal imepania kuhakikisha inasajili mshambuliaji mpya katika kipindi hiki cha usajili na katika kuhakikisha hilo linafanikiwa imeripotiwa kuwa tayari kutoa kitita cha €40m ili kumsajili mshambuliaji wa Lyon,Alexandre Lacazette,25, aliyefunga mabao 23 msimu uliopita.(Daily Telegraph)
Van Persie:Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United,Robin Van Persie,32,ameripotiwa kuwa katika mzungumzo na klabu ya Middlesbrough ili kuangalia uwezekano wa kujiunga nayo msimu huu.Tayari nyota mwingine wa Manchester United,Victor Valdes,34,ameshafikia makubaliano na klabu hiyo na Alhamis atafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu.( The Daily Mail)
Schweinsteiger:Paris Saint-Germain inataka kumsajili kiungo mkongwe wa Manchester United,Mjerumani Bastian
Schweinsteiger,32,ili kumfanya kiongozi wake mpya uwanjani hii ni baada ya kuondoka kwa Zlatan Ibrahimovic,34.(Sport Bild)
Bonucci:Manchester City imekwaa kisiki katika mbio zake za kumuwania mlinzi wa kati wa Italia,Leonardo Bonucci baada ya ofa yake ya £38m kukataliwa na klabu yake ya Juventus. Bonucci,29,ameichezea Juventus michezo zaidi ya 250 akifanikiwa kufunga mabao 30 huku akitwaa mataji matano ya Serie A.(Daily Mail)
Bakayoko:Manchester United imeripotiwa kuvutiwa na kiungo wa Monaco,Tiemoue Bakayoko na huenda ikamsajili katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Mbali ya Manchester United vilabu vingine vinavyomuwania Bakayoko,21, ni Stoke City pamoja na Southampton.(AS)
Bielsa:SS Lazio imemtangaza,Marcelo Bielsa kuwa kocha wake mpya na ataanza kuinoa klabu hiyo ya jiji la Roma kuanzia Julai 9.(Gazzetta dello Sports)
Vermaelen:Liverpool imeripotiwa kutenga ofa ya £12m kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa Barcelona,Mbelgiji Thomas Vermaelen,30,ambaye mara kadhaa ameripotiwa kuwa na mpango wa kutaka kurudi England.(Mundo Deportivo)
0 comments:
Post a Comment