Lille,Ufaransa.
MLINZI wa zamani wa TP Mazembe,Mzambia,Stoppila Sunzu,amejiunga na Lille kwa kandarasi ya miaka mitatu akitokea Shanghai Shenhua ya China.
Sunzu,27, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Zambia kilichotwaa ubingwa wa AFCON mwaka 2012 amejiunga na Lille maarufu kama Les
Dogues baada ya kufanya vizuri msimu uliopita wakati akiitumikia klabu hiyo kwa mkopo.
Msimu uliopita,Sunzu,aliichezea Lille jumla ya michezo 16 na kufanikiwa kufunga mabao mawili.Kabla ya kutua Lille,Sunzu,pia aliwahi kuichezea Sochaux ya Ufaransa kabla ya kutimkia Shanghai Shenhua.
0 comments:
Post a Comment