Cairo,Misri.
SHIRIKISHO la soka Afrika (CAF) limetangaza kumfungia kwa muda wa miaka miwili,kiungo wa Congo DR na AS Vita Club,Christian Ngudikama,baada ya kumkuta na hatia ya kutumia madawa yaliyopigwa marufuku michezoni.
Taarifa kutoka CAF zimesema Ngudikama,28, alitiwa hatiani mwezi Januari mwaka huu baada ya vipimo kuonyesha kuwa alitumia dawa aina ya ephedrine ambayo hutumika kusisimua misuli wakati akiitumikia Congo DR katika michuano ya CHAN iliyofanyika nchini Rwanda.
CAF pia imethibitisha kumfungia kwa kipindi cha miaka miwili pamoja na kumtoza faini ya Dola 25,000,Makamu wa Rais wa chama cha soka cha Equatorial Guinea's Football Federation,
Gustavo N'dong Edu,baada ya kumkuta na hatia ya kujaribu kutoa hongo kwa mwamuzi katika mchezo dhidi ya Mali katika michuano ya Afcon kwa upande wa wanawake.
Katika adhabu nyingine,CAF imetangaza kumfungia kwa kipindi cha miezi sita nyota wa Al Merreikh,Alaa Eldin
Youssef,kwa kosa la kumpiga mpiga picha.
Pia CAF imeitoza faini ya Dola 45,000 klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia baada ya mashabiki wake kuwafanyia fujo na kuwatishia maisha wachezaji wa Enyimba ya Nigeria katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika ulioisha kwa sare ya mabao 3-3 na Wageni Enyimba kushinda kwa mikwaju ya penati.
0 comments:
Post a Comment