Southampton, England.
KLABU ya Southampton imetangaza kukamilisha usajili wa Kiungo wa Denmark,Pierre-Emile Hojbjerg,kutoka Bayern Munich ya Ujerumani kwa ada ya Paundi Milioni 12.
Hojbjerg,20,amesaini Mkataba wa Miaka Mitano wa kuitumikia Miamba hiyo ya St.Mary's hii ni baada ya kufaulu vipimo vyake vya Afya.
Hojbjerg alijiunga na Bayern Munich mwaka 2012 akitokea Brondby ya nyumbani kwao Dermark wakati huo akiwa kinda wa miaka 17.
Msimu uliopita,Hojbjerg, aliichezea Schalke kwa mkopo ambapo alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 30 ya Ligi ya Bundesliga.
Hojbjerg anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Southampton katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya,wa kwanza alikuwa ni Nathan Redmond aliyejiunga akitokea Norwich City.
0 comments:
Post a Comment